
Na Godfrey Marwa, Tarime

Mteule wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Petro Fanuel Makorere, leo Agosti 27, 2025 amerejesha fomu ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuomba kuteuliwa kugombea udiwani wa kata ya Nyarero katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime [Vijijini], mkoani Mara.
Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu hiyo kwenye ofisi za INEC Kata ya Nyarero, Makorere amesema: "Nawaomba wana-Nyarero mmpe Dkt. Samia Suluhu Hassan kura, Mbunge Waitara na mimi, mtuunge mkono tuwe na mafiga matatu kwenda kutekeleza ilani ya CCM na kuwaletea maendeleo."
Makorere ameongeza: "Naenda kusaidia kata yetu kimaendeleo, kuhakikisha vijana wanafuata nyayo za elimu, kuangalia afya, miundombinu, ikiwemo ya barabara kwenye vitongoji vyetu, pia vitongoji ambavyo havijapata umeme na maji, kilimo tunaenda kuangalia pembejeo zipatikane pamoja na masoko.”

Petro Fanuel Makorere (wa pili kulia) akirejesha fomu ya udiwani katika ofisi za INEC Kata ya Nyarero wilayani Tarime leo. (Picha zote na Mara Online News)
------------------------------------
Naye Diwani aliyemaliza muda wake, John Mohabasi Marwa, amesema: "Tukishapata kiongozi mpya ndani ya chama makundi yote yanahamia kwa ambaye ameteuliwa na chama, na mimi kundi langu tunahamia kwa Fanuel Makorere kuhakikisha CCM kinapata kura kwake kama diwani, Mbunge Waitara na Rais Samia.”
"Niwaombe wana-CCM wote kata ya Nyarero tuwe wamoja, tuunde mnyororo - diwani aliyekuwa madarakani akiondokani miradi ambayo haijakamilika – diwani anayekuja ataiendeleza," ameongeza Mohabasi.
No comments:
Post a Comment