NEWS

Wednesday, 20 August 2025

Salah, Rogers washinda Tuzo za Chama cha Wanasoka wa Kulipwa



Mohamed Salah

Winga wa Liverpool, Mohamed Salah, ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Chama cha Wanasoka wa Kulipwa (PFA), huku kiungo wa Aston Villa, Morgan Rogers, akichaguliwa kuwa mchezaji bora chipukizi wa mwaka.

Morgan Rogers

Meneja wa zamani wa England, Sir Gareth Southgate, naye ameshinda Tuzo ya PFA 2025 kwa mchango wake katika soka na mafanikio akiwa na timu ya taifa.

Salah, 33, ndiye mchezaji wa kwanza kushinda tuzo hiyo mara tatu, baada ya kuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya Liverpool msimu uliopita.

Alipoulizwa kama alikuwa na matamanio ya kushinda tuzo wakati akikulia Misri, alisema: "Ni kweli nilitaka kuwa mchezaji wa mpira wa soka na nilitaka kuwa maarufu na kutunza familia yangu, lakini hufikirii mambo makubwa wakati bado uko Misri.

"Unapokua, unaanza kuona mambo kwa njia tofauti, kuwa na tamaa na unaanza kuwa na mtazamo mpana."

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri, alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu wa 2024-25.

Mchezaji mwenzake wa Reds, Alexis Mac Allister, nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes, mshambuliaji wa Newcastle, Alexander Isak, mshambuliaji wa Chelsea, Cole Palmer na kiungo wa kati wa Arsenal, Declan Rice, pia walikuwa kwenye orodha ya walioteuliwa.
Chanzo: BBC Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages