
Kutoka kushoto ni makadawa wa CCM, Mgore Miraji Kigera na Mary Joseph Daniel.
---------------------------------------
Katika kile kinachoonekana kama kuimarika kwa ushiriki wa wanawake katika kugombea nafasi za uongozi wa kisiasa, makada wanawake wawili wameibuka washindi katika kura za maoni za ubunge ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mara.
Wanawake hao na majimbo yao yakiwa kwenye mabano, ni Mwenmyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Mara, Mary Joseph Daniel (Serengeti) na Mjumbe wa Baraza la Wazazi CCM Taifa, Mgore Miraji Kigera (Musoma Mjini), wote ikiwa ni mara yao ya kwanza kujitupa katika kinyang’anyiro hicho.
Kura za maoni za wajumbe ni sehemu ya mchakato wa ndani wa CCM kuelekea kuwapata wagombea wa ubunge watakaopeperusha bendera ya chama hicho tawala katika Uchaguzi Mkuu unaotarajuiwa kufanyika nchgini Oktoba 29, 2025.
Makada wengine walioibuka kidedea katika kura za maoni ndani ya CCM mkoani Mara ni Prof. Sospeter Muhongo (Musoma Vijijini), Jafari Chege (Rorya), Michael Kembaki (Tarime Mjini), Mwita Waitara (Tarime Vijijini), Dkt. Wilson Mahera (Butiama) na Robert Maboto (Bunda Mjini).
No comments:
Post a Comment