NEWS

Wednesday, 6 August 2025

Spika mstaafu Job Ndugai afariki dunia jijini Dodoma


Job Ndugai enzi za uhai

Na Mwandishi Wetu

Spika mstaafu Job Yustino Ndugai amefadiki dunia jijini Dodoma leo Agosti 6, 2025, kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Umoja wa Mabunge Duniani, Dkt. Tulia Ackson.

Kwa masikitiko makubwa, naomba kutoa taarifa ya kifo cha kiongozi wetu, mwanasiasa mkongwe na Spika Mstaafu wa Bunge Mheshimiwa Job Yustino Ndungai kilichotokea leo jijini Dodoma.

"Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa jimbo la Kongwa, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu," amesema Spika Tulia katika taarifa hiyo ambayo imeeleza kuwa ofisi yake inashirikiana na Kamati ya Mazishi na familia ya marehemu kuratibu mipango ya mazishi.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages