NEWS

Friday, 29 August 2025

Mgombea Mwenza wa Urais Dkt. Nchimbi kuzindua kampeni za Uchaguzi Mkuu za CCM mkoani Mara Jumapili



Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi (kushoto) 
na Patrick Chandi Marwa
--------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Mara

Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, anatarajiwa kuzindua kampeni za Uchaguzi Mkuu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mara kesho kutwa Jumamosi.

“Mheshimiwa Balozi Dkt. Nchimbi atawasili mkoani kwetu tarehe 30 Agosti mwaka huu na ziara yake ya kuzindua kampeni za Uchaguzi Mkuu za chama,” Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa, aliimbia Mara Online News kwa njia ya simu jana Ijumaa.

Kwa mujibu wa Chandi, Balozi Dkt. Nchimbi ambaye ni Mgombea Mwenza wa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kinyang’anyiro cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atakapowasili atapata fursa ya kusalimia wananchi wa wilaya ya Bunda na Kiabakari wilayani Butiama,

Agosti 31, Dkt. Nchimbi ataanza kuhutubia mikutano ya kampeni katika mji wa Nyamongo - Tarime Vijijini na baadaye mjini Tarime kabla ya kuhutubia mkutano mkubwa wilayani Rorya.

“Ninatoa wito kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wa CCM na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kumsiskiliza mgombea Mwenza wa Urais wa CCM,” alisema Chandi.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages