NEWS

Thursday, 14 August 2025

Rais Samia atunukiwa Tuzo ya Kimataifa 2025 kwa ubunifu wa mageuzi makubwa sekta ya maji



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizindua mradi wa maji nchini.
-------------------------------------

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Tuzo ya Rais ya Kimataifa ya Wabunifu wa Mabadiliko katika Sekta ya Maji 2025 (Presidential Global Water Changemakers Award 2025), ikiwa ni heshima kubwa inayotolewa na Taasisi ya Maji Duniani (Global Water Partnership) kwa ushirikiano na Umoja wa Afrika (AU).

Tuzo hiyo ilitolewa rasmi na Rais Duma Boko wa Jamhuri ya Botswana, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tuzo za Rais za Kimataifa za Wabunifu wa Mabadiliko katika Sekta ya Maji 2025, ambapo kwa niaba ya Rais Samia, tuzo ilipokewa na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, James Bwana.

Tuzo hiyo ilitolewa wakati wa Mkutano wa Kilele wa Uwekezaji katika Sekta ya Maji wa AU-AIP 2025, ulioanza jijini Cape Town, Afrika Kusini, unaotarajiwa kumalizika leo Agosti 15, 2025.

Global Water Partnership imetambua uongozi bora na jitihada za mageuzi za Rais Samia katika sekta ya maji, ikiwemo uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya maji, upanuzi wa huduma ya maji safi kote nchini Tanzania, pamoja na mikakati bunifu ya ufadhili, kama vile Hatifungani ya Kijani (Green Bond).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages