
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA, Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali George Marwa Waitara, akipokea Tuzo kutoka kwa Mjumbe wa Bodi hiyo, Dkt. Robert Fyumagwa.
------------------------------------
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali George Marwa Waitara, amepokea Tuzo iliyotolewa na shirika hilo kutambua mchango wake katika kuendeleza na kusimamia shughuli za uhifadhi nchini.
Jenerali Mstaafu Waitara alikabidhiwa tuzo hiyo jana Agosti 14, 2025 na Mjumbe wa Bodi ya TANAPA, Dkt. Robert Fyumagwa, ambaye aliipokea kwa niaba yake wakati wa maadhimisho ya Siku ya Askari Wanyamapori Duniani (World Ranger’s Day) yaliyofanyika Julai 31, 2025 katika Hifadhi ya Taifa Tarangire.

No comments:
Post a Comment