NEWS

Tuesday, 26 August 2025

Serikali yaelekeza nguvu kwenye ujenzi wa maabara za madini nchini


Waziri wa Madini, Anthony Mavunde 
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema ujenzi wa maabara za kiasa za utafiti na uchambuzi wa sampuli za madini utakuwa nguzo kubwa ya kisayansi itakayowasaidia wachimbaji wadogo kuongeza ufanisi na kuwapunguzia gharama na usumbufu wa kusafiri ili kufuata huduma hizo sehemu nyingine nchini.

Maabara hizo zitajengwa ili kusaidia wachimbaji wadogo katika kuimarisha mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa taifa.

Hayo yameelezwa Alhamis wiki hii na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa maabara ya kisasa ya utafiti na uchambuzi wa madini inayojengwa mkoani Geita kwa thamani ya shilingi bilioni 3.5.

Maabara ya Geita inatazamiwa kuwahudumia wachimbaji wa Kanda ya Ziwa inayojummuisha mikoa ya Geita, Kagera, Mwanza, Shiynaga, Simiyu na Mara.

Maaabara nyingine za kisasa zitajengwa Chunya, mkoani Mbeya wakati maabara kubwa zaidi ya kimataifa itajengwa jijijini Dodoma.

Azma ya serikali kwa sasa ni kuimarisha sekta ya madini ili iweze kutoa mchjango mkubwa katika uchumi wa Tanzania, hasa baada ya kujaliwa kuwa na aina nyingi ya madini yanayohitajika duniani kote.

Kwa sasa Taaisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ndiyo kitovu cha shughuli za madini hapa nchini kwa kazi za utafiti wa jiolojia na kwamba kuanzishwa kwa maabara ya Geita kutachochea shughuli za madini katika ukanda wa Ziwa ambao unaongoza kwa uchimbaji hapa Tanzania – hasa mikoa ya kimadini ya Mbogwe, Geita, Kagera, Mwanza, Kahama, Mara na Shinyanga.

Kwa mujibu wa Mavunde, mwaka jana serikali ilikusanya maduhuli ya shilingi bilioni 328 kutoka mkoa wa kimadini wa Geita

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela, alisema ujenzi wa maabara ya madini mkoani mwake utawapunguzia wananchi muda na gharama ya kusafiri kwenda Dodoma kufuata huduma za uchambuzi.

Naye Mkurugenzi wa huduma za maabara wa GST, Notika Bandeze, alisema maabara ya Geita itakuwa na vifaa vya kisasa vya utambuzi wa madini na uchunguzi wa sampuli pamoja na utoaji wa taarifa za kina za kijiolojia.

Imechukua muda wa karne moja kwa GST kujielekeza kwenye ujenzi wa maabara za uchambuzi na uchunguzi wa madini, kwa mujibu wa taarifa ya taasisi hiyo.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages