Kufuatia mkutano wa Rais wa Marekani, Donald Trump na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, kumalizika bila makubaliano, Trump sasa anatarajia kukutana na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky.
Hata hivyo, katika ujumbe wake kwenye Truth Social Platform, Trump amesema "mazungumzo yao yalikuwa yenye tija huko Alaska".
Hatua hizo zinalenga kutafuta njia bora ya kumaliza vita ya kutisha kati ya Urusi na Ukraine kwa mazungumzo ya amani.
"Kama yote yatafanyika hivyo, basi tutapanga mkutano na Rais Putin. Kuna uwezekano mkubwa maisha ya mamilioni ya watu yataokolewa," amesema Trump.
Rais Zelensky amesema atakutana na Trump kwa mazungumzo huko Washington DC, Marekani siku ya Jumatatu ijayo.
Katika ujumbe kwenye mtandao wa Telegraph, Zelensky amesema "anashukuru kwa mwaliko."
Zelensky amesema raia wa Ukraine hawakufurahishwa sana na kuachwa nje ya mkutano wa Trump na Putin huko Alaska, na kusisitiza katika taarifa hiyo kwamba viongozi wote watatu wanapaswa kuwepo kwa duru inayofuata ya mazungumzo.
Pia, amesisitiza umuhimu wa viongozi wa Ulaya kuwepo "katika kila hatua."
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment