Na Mwandishi Wetu
Serikali ya Norway imetoa shilingi bilioni 4.5 kwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Lhrc) kukiimarisha kiendelee kusaidia jamii katika masuala ya kutetea haki, demokrasia, elimu kwa umma, mabadiliko ya sera na utetezi wa masuala ya jinsia.
Hafla ya kutiwa saini mkataba huo wa miaka mitatu wa makabidhiano ya fedha hizo ilifanyika Jumatatu.wiki hii jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Fulgence Masawe, alisema serikali ya Norway ni mdau muhimu anayeunga mkono utekelezaji wa shughuli za kituo hicho.
”Tumeingia mktaba wa miaka mitatu na Norway kutusaidia katika shughuli zetu kama vile msaada wa kisheria na mambo mengine muhimu yanayoakisi majukumu yetu,” alisema.

No comments:
Post a Comment