Na Mwandishi Wetu
Watu sita wamefariki mkoani Mara baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka wilaya ya Tarime kwenda wilaya ya Rorya kuparamia gari jingine lililokuwa limeharibika na kuegeshwa kando ya barabara.
Ajali hiyo, iliyohusisha gari lenye namba za usajili T.625 DYV aina ya Probox, imetokea alfajiri ya kuamkia leo katika kijiji cha Konga, kata ya Bukwe, wilayani Rorya.
Mashuhuda wa ajali wamesema marehemu, ambao majina yao bado hayajatambuliwa mpaka sasa, walikuwa ni wafanyabiashara waliokuwa wakielekea mwalo wa Busurwa wilayani Rorya.
Wamesema kwamba majeruhi mmoja alikimbizwa kwenda hospitalini kwa matibabu baada ya kutokea ajali hiyo mbaya iliyohusisha gari jingine lenye namba za usajili T. 857 BRX aina ya Fuso ambalo liliharibika na kugeshwa kando ya barabara.
Mashuhuda hao walisema kwamba wanasubiri taarifa za polisi kuhusu uchunguzi wa tukio hilo la kusikitisha.
No comments:
Post a Comment