![]() |
| Katibu Mtendaji wa Necta, Profesa Said Mohamed |
Na Mwandishi Wetu
Watahiniwa 1,172,279 wanaomaliza Darasa la Saba leo Jumatano Agosti 10, 2025 wameanza kufanya mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi ambayo itamalizika kesho na Alhamis Agosti 11, 2025.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Profesa Said Mohamed, alitangaza jana kwamba idadi ya watahiniwa hao wanatoka shule 19,441 nchini ambapo kati yao ni wavulana 535,138 (asilimia 46) na wasichana 637,141 (asilimia 54).
Alisema kati ya watahiniwa wote, idadi ya wanafunzi walemavu watakaofanya mitihani yao watakuwa 4,6766. Idadi hiyo ya wanafunzi walemavu inajumuisha wale wasioona, wenye uoni hafifu, na wenye changamoto za uziwi.
Kwa mujibu wa Prof Mohamed, masomo yatakayotumika kuwapima wanafunzi ufahamu wao ni Kiswahili, Kiingereza, Hisabati, Sayansi na Teknolojia, Maarifa ya Jamii, Stadi za Kazi na uraia.

No comments:
Post a Comment