NEWS

Saturday, 27 July 2024

Mwenge wa Uhuru wazindua jengo la Nyamongo Plaza




Na Godfrey Marwa, Nyamongo
------------------------------------------

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Eliakimu Mnzava, amezindua jengo la kisasa la Nyamongo Plaza lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, mkoani Mara.

Jengo hilo la ghorofa mbili, ni mali ya mfanyabiashara Josephat Mwita lililojengwa kwa ajili ya shughuli za kibiashara katika mji wa Nyamongo, jirani na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara.

Akizungumza mara baada ya kuzindua jengo hilo leo Julai 27, 2024, Mnzava alimpongeza mfanyabiashara huyo, akisema ni kielelezo cha ushiriki wa sekta binafsi katika kuchangia ukuzaji wa uchumi nchini.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Eliakimu Mnzava (wa pili kushoto) akizindua jengo la Nyamongo Plaza. Kushoto ni mmiliki wa jengo hilo, Josephat Mwita na kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Tarime, Mwalimu Saul Mwaisenye. (Picha na Mara Online News)
--------------------------------------------------

“Tunampongeza Mwita kwa kazi nzuri. Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kafungua milango ya uwekezaji na biashara, hapa huyu analipa kodi, serikali itakusanya mapato kutoka kwenye jengo hili,” amesema Mnzava.

Aidha, Mnzava amemkabidhi mfanyabiashara huyo Mwenge wa Uhuru kama ishara ya serikali kutambua ushiriki wake katika uwekezaji na biashara kupitia sekta binafsi.

Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa pia amejionea uendelevu wa mradi mkubwa wa majisafi na salama ya bomba uliotekelezwa chini ya usimamizi wa RUWASA katika kijiji cha Nyangoto, Nyamongo kutokana na fedha za Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR) kutoka mgodi wa Noth Mara.

Mfanyabiashara Josephati Mwita (katikati) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru. (Picha na Mara Online News)
-------------------------------------------------
Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages