Katibu Tawala wa Wilaya ya Tarime, Mwalimu Saul Mwaisenye (kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Serengeti, Angelina Marko. Makabidhiano hayo yamefanyika kijijini Kerende katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) mapema leo Julai 27, 2024 asubuhi. (Picha na Mara Online News)
------------------------------------------------
-------------------------------------
Baada ya kuhitimisha mbio zake katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti jana, Mwenge wa Uhuru umewasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) mkoani Mara.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Serengeti, Angelina Marko amekabidhi Mwenge huo kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Tarime, Mwalimu Saul Mwaisenye katika kijiji cha Kerende mapema leo Julai 27, 2024 asubuhi.
Mwenge wa Uhuru uliwasili mkoani Mara jana Julai 26, 2024 ambapo utakimbizwa katika wilaya sita na halmashauri tisa katika umbali wa kilomita zaidi ya 1,000.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Alfred Mtambi, Mwenge huo utapita katika miradi ya maendeleo 72 yenye thamani ya shilingi bilioni 24.961, ambayo imetekelezwa kutokana na michango iliyotolewa na wananchi, halmashauri, Serikali Kuu na wahisani.
Kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2024 inayosema: “Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu.”
No comments:
Post a Comment