Rais Paul Kagame wa Rwanda akiwa anapiga kura katika uchaguzi wa mkuu huu Rwanda
-------------------
Katika taarifa ya awali, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) huko Kigali ilisema kwamba Kagame alishinda kwa kishindo wapinzani wake wawili, ambao walionekana kuwa na nafasi ndogo ya kushinda, akipata asilimia 99 ya kura.
Kiongozi mwenye umri wa miaka 66 aligombea kiti hicho akiwakilisha chama cha Rwandan Patriotic Front (RPF) dhidi ya Frank Habineza wa Chama cha Democratic Green na Philippe Mpayimana, mgombea huru.
Tume hiyo, ikionyesha uwazi na ufanisi, ilisema kwamba asilimia 21.06 ya kura zilikuwa hazijahesabiwa bado. Kufikia jioni ya Jumatatu, Julai 15, Kagame alikuwa amepata zaidi ya kura milioni 7.
Habineza alikuwa nyuma sana akipata kura 38,301, sawa na asilimia 0.53, wakati Mpayimana alikuwa wa tatu kwa kura 22,753 (asilimia 0.32). Baada ya Kagame kutangazwa mshindi, atakuwa Raisi kwa miaka mingine mitano.
CHANZO:KTN NEWS.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
- 1.Sababu za Halmashauri ya Serengeti kupata hati ya ukaguzi yenye mashaka .
- 2. Musoma Vijijini wanavyopiga hatua ujenzi shule za sekondari za kata .
- 3.Rais Samia atembelea Sekondari ya Seminari ya Kaengesa mkoani Rukwa .
- 4. HAIPPA PLC inavyoshagihisha uwekezaji Tanzania .
- 5.Mwanahabari kumlipa fidia Waziri Mkuu wa Italia baada ya kufanya mzaha juu ya kimo chake .
No comments:
Post a Comment