NEWS

Monday, 27 January 2025

Viongozi wa Afrika wakutana Tanzania kujadili kuhusu nishati



 
Wakati Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati ukianza leo jijini Dar es Salaam, ulinzi na usalama umeimarishwa katika maeneo mbalimbali huku shughuli mbalimbali za kiuchumi zikiendelea.

Alkadhalika usafiri nafuu yaani bajaji na bodaboba umesitishwa kwa baadhi ya maeneo ya jiji baada ya kuzuiwa kuingia katikati ya jiji kwa siku mbili.

Kufuatia tamko la juzi, barabara kuu tisa zinazoelekea katika jiji hilo zimefungwa, shule za umma na nyingine za binafsi zimefungwa pamoja na shughuli mbalimbali katika ofisi za umma nazo zimesimama huku watumishi wa umma wakihimizwa kufanya kazi majumbani.

Kwa mujibu wa wataalamu wa kiuchumi, ujio wa ugeni mkubwa wakiwemo wakuu wa nchi na viongozi wa taasisi kubwa ulimwenguni utaitangaza Tanzania na fursa zake, hivyo kurahisisha kupatikana kwa wawekezaji na hatimaye kuzalisha ajira.

Kwa mujibu wa nchi mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, mkutano huo unalenga kuongeza uunganishaji nishati kwa Waafrika milioni 300 ifikapo mwaka 2030.

Zaidi ya wakuu wa nchi 25 na mawaziri 60 wanatarajiwa kuwa sehemu ya mkutano huo wa siku mbili.
Chanzo:BBC
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages