NEWS

Friday, 24 January 2025

Barrick North Mara yakabidhi bilioni 3.7/- za ‘service levy’ Tarime Vijijini, bilioni 1.7/- za mrabaha kwa vijiji vitano



Rais na CEO wa Barrick, Dkt Mark Bristow akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi bilioni 3.7 kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime katika ukumbi wa mikutano wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara jana Januari 24, 2025.
----------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Tarime

Mgodi wa Dhahabu wa North Mara umeipatia Halmashairi ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) shilingi bilioni 3.709, ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma (service levy) ya mwaka wa fedha 2023/2024.

Wakati huo huo, mgodi huo umevipatia vijiji vitano gawio la mrabaha la shilingi bilioni 1.718 ambazo ni malipo ya robo ya nne ya mwaka 2024.

Vijiji hivyo na kiasi cha fedha kilichopokewa kikiwa kwenye mabano ni Genkuru (749,488,891), Nyangoto (635,141,742), Kerende (195,749,927), Nyamwaga (95,529,025) na Kewanja (42,254,479).

Rais na CEO wa Barrick, Dkt Mark Bristow (katikati waliokaa), Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara (wa tatu waliokaa), Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri, Petro Kurate (wa pili waliokaa), viongozi wa kata na vijiji, na wafanyakazi wa mgodi wa North Mara wakifurahia picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano ya mifano ya hundi za malipo ya 'service levy' na mrabaha jana.
-----------------------------------------


Rais na CEO wa Barrick, Dkt Mark Bristow akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 195.749 kwa viongozi wa kijiji cha Kerende jana.
----------------------------------

Rais na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Barrick, Dkt Mark Bristow alikabidhi mifano ya hundi za malipo hayo ya ushuru wa huduma na mrabaha kwa viongozi husika jana Januari 24, 2025, wakati wa kikao chake na Kamati ya Maendeleo ya Jamii (CDC) inayoundwa kwa sehemu kubwa na viongozi wa vijiji 11 vilivyo jirani na mgodi huo.

Viongozi wa halmashauri na vijiji waliushukuru mgodi wa North Mara na kuahidi kwenda kusimamia vizuri matumizi ya mabilioni hayo ya fedha ili kuchochea maendeleo ya wananchi, hasa katika ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya huduma za kijamii.

“Tunaushukuru sana mgodi kutupatia fedha hizi, na sisi kama viongozi tunaahidi kwamba zitakwenda kufanya kazi iliyokusudiwa,” alisema Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Petro Kurate.


Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Meneja Mkuu wa Mgodi, Apolinary Lyambiko na Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara ambaye aliwataka viongozi wa halmashauri na vijiji kushirikisha wananchi katika matumizi ya fedha hizo.

Mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaendeshwa na kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni tanzu ya Twiga Minerals.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages