NEWS

Tuesday, 23 July 2024

Rais Samia ang'oa vigogo TTCL, Posta na Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote



Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
-------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu
----------------------------

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa viongozi mbalimbali wa mashirika matatu nchini.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt Moses Kusiluka leo Julai 23, 2024, imewataja viongozi hao kama ifiatavyo:

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Zuhura Sinare Muro na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Mhandizi Peter Rudolph Ulanga.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania, Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Ocholla Mabongo na Postamasta Mkuu wa shirika hilo, Maharage Aly Chande.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Prof John Nkoma na Afisa Mtendaji Mkuu wa mfuko huo, Justina Tumaini Mashiba.
Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages