NEWS

Friday, 2 August 2024

Mwenge wa Uhuru kumulika miradi ya maendeleo Bunda leo



Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dkt Vicent Naano (kushoto) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Moses Kaegele mapema leo asubuhi.
---------------------------------------------

Na Godfrey Marwa, Bunda
------------------------------------

Mwenge wa Uhuru umeingia Halmashauri ya Wilaya ya Bunda baada ya kukamilisha mbio zake katika Halmashauri ya Wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dkt Vicent Naano amepokea mwenge huo mapema leo asubuhi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Moses Kaegele.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Eliakimu Mnzava atakagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Katika mbio za wilayani Butiama jana, Mnzava alitumia Mwenge wa Uhuru kuwasha Mwenge wa Mwitongo nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2024, Godfrey Eliakimu Mnzava (mwenye mwenge) na msafara wake wakiwa Mwitongo wilayani Butiama nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere jana, ambapo alitumia mwenge huo kuwasha Mwenge wa Mwitongo. Kulia mbele ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Gerald Musabila Kusaya na kushoto ni mtoto wa Mwalimu Nyerere, Madaraka Nyerere. (Picha zote na Mara Online News)
-----------------------------------------------

Mbali na kuwasha Mwenge wa Mwitongo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 na msafara wake waliwasilisha salamu kwa familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na kuzuru kaburi lake.
Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages