NEWS

Thursday 1 August 2024

Kiongozi Mwenge wa Uhuru 2024 awasha Mwenge wa Mwitongo, RC Mara asisitiza kumuenzi Mwalimu Nyerere



Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Eliakimu Mnzava akiongoza wenzake kuwasha Mwenge wa Mwitongo kwa kutumia Mwenge wa Uhuru leo Agosti 1, 2024.
---------------------------------------------

Na Godfrey Marwa, Butiama
---------------------------------------

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Eliakimu Mnzava amewasha Mwenge wa Mwitongo nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Katika tukio hilo la leo Agosti 1, 2024, Mnzava ametumia Mwenge wa Uhuru kuwasha Mwenge wa Mwitongo katika wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mkuu wa Mkoa (RC) wa Mara, Kanali Evans Alfred Mtambi amewasisitiza wananchi wa mkoa wa huo kuendelea kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kutunza mazingira, kudumisha amani na upendo pamoja na kushiriki uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
RC Mtambi akizungumza Mwitongo 
wilayani Butiama
--------------------------------------------

“Mwenge wa Mwitongo umetimiza miaka 60, kwetu wana-Mara hii ni faraja kubwa kuona tukio hili likiendelea, na kama inavyojulikana Mwalimu Nyerere alipenda Taifa lake, aliyokuwa anayafanya ilikuwa kwa moyo wake wa dhati na alipenda kutunza mazingira.

"Sisi kama wana-Mara tumelichukulia hili kama bahati kwetu, tumuenzi Mwalimu, alipenda watu wake bila ubaguzi wa aina yoyote na tuchukie dhuluma,” amesema RC Mtambi.

Mbali na kuwasha Mwenge wa Mwitongo, Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 na msafara wake wamefika Mwitongo kuwasilisha salamu kwa familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na kuzuru kaburi lake.
Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages