
Timu ya Benki ya Dunia iliyoambatana na wajumbe kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakikagua ujenzi wa Kampasi Kuu Butiama ya Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia, Ijumaa iliyopita.
----------------------------------------------
Benki ya Dunia (WB) imetembelea Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) na kukagua maendeleo ya ujenzi unaotekelezwa na chuo kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).
Ziara hiyo ilifanyika Ijumaa iliyopita katika Kampasi Kuu iliyopo Butiama, ikiongozwa na Prof Roberta Malee wa WB aliyeambatana na QS Nkahiga Mathus Kaboko na wajumbe wengine kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Ugeni huo umefurahishwa kwa maendeleo mazuri ya ujenzi huo na kukipongeza chuo kwa kazi inayoendelea kwamba ni kubwa kuliko walivyotegemea.
“Tumeridhishwa sana na kujivunia kwa hatua hii ambayo imefikiwa na MJNUAT katika ujenzi wa kampasi hii. Ubora wa majengo unavutia na kasi ya ujenzi ipo vizuri. Mwaka mmoja na nusu uliopita hapa hapakuwa na chochote lakini leo tunaona hatua hii iliyofikiwa,” alisisitiza Prof Roberta Malee.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof Lesakit Mellau aliueleza ugeni huo kwamba chuo kinaendelea kufanya jitihada za kutekeleza mradi wa HEET na kukabiliana na changamoto zinazojitokeza ili kuhakikisha kuwa ujenzi huo unafikia malengo.
“Tunashirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Benki ya Dunia na taasisi nyingine za elimu ya juu kuhakikisha kwamba mradi huu unakamilika kwa muda uliowekwa,” alieleza Prof Mellau.
Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia ni miongoni mwa taasisi 23 zinazonufaika na Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) ambao ni mkopo kutoka Benki ya Dunia kwenda kwa Serikali ya Tanzania.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>MAKALA:Mwenyekiti Halmashauri Tarime Vijijini ataja miradi ya bilioni 9/- za CSR Barrick North Mara
>>CHADEMA Tarime Mjini wajitabiria ushindi Serikali za Mitaa, Kada wa CCM Musoma Mjini amwaga manyanga
>>Man United yamtimua Kocha Ten Hag
>>MAKALA MAALUMU:Ajenda ya nishati safi ya kupikia na ugumu wa biashara ya mkaa mjini Bukoba
No comments:
Post a Comment