NEWS

Monday, 28 October 2024

CHADEMA Tarime Mjini wajitabiria ushindi Serikali za Mitaa, Kada wa CCM Musoma Mjini amwaga manyanga



Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Tarime Mjini, 
Bashiri Abdallah Selemani "Sauti".
---------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

Chama cha upinzani - CHADEMA Jimbo la Tarime Mjini kimejitabiria ushindi wa zaidi ya nusu ya mitaa yote 81 katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini kote Novemba 27, mwaka huu.

“Tumeshawapata wagombea wa mitaa yote 81, tathmini yetu inaonesha tutashinda katika mitaa 50 hadi 65,” Mwenyekiti wa CHADEMA wa jimbo hilo, Bashiri Abdallah Selemani maarufu kwa jina la Sauti aliiambia Mara Online News kwa njia ya simu jana.

Wakati huo huo, kada wa chama tawala - CCM, Ally Zedi Rajabu amehamia CHADEMA baada ya kushindwa kwenye kura za maoni za kuwania uenyekiti mtaa wa Kitaji katika jimbo la Musoma Mjini akidai ‘kuchezewa rafu’.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages