
Rigathi Gachagua
Mahakama Kuu nchini Kenya imeondoa amri zinazomzuia Naibu Rais Mteule Kithure Kindiki kuapishwa.
Wakati wakitoa uamuzi huo, jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Eric Ogola, Anthony Mrima na Fredah Mugambi walisema nafasi ya kikatiba ya naibu rais haiwezi kuachwa wazi.
David Munyi Mathenge na Peter Gichobi Kamotho walitaka mahakama kuweka maagizo ya kusitisha kuapishwa kwa Kindiki Kithure kama Naibu Rais mpya baada ya Bunge la Kitaifa kuidhinisha uteuzi wake, siku moja baada ya Bunge la Seneti kupiga kura ya kumtimua Rigathi Gachagua.
David Munyi Mathenge na Peter Gichobi Kamotho walitaja suala hilo kuwa la "umuhimu mkubwa na udharura wa kitaifa."
Wakitoa uamuzi wao, jopo la majaji watatu waliendelea kusema kwamba kesi hiyo itatajwa Novemba 7, 2024, na kuongeza kuwa Gachagua yuko huru kuwasilisha rufaa dhidi ya uamuzi huo.
"Maombi ya maagizo ya kumzuia Naibu Rais Mteule Kithure Kindiki kuapishwa yamekataliwa.
Maagizo hayo yaliyotolewa Oktoba 18, 2024 katika Mahakama Kuu ya Kerugoya yanaondolewa, au kuwekwa kando.
Kuna uhuru wa kukata rufaa. Nakala za maelezo ya kesi hii yaliyochapishwa na nakala zilizoidhinishwa za uamuzi huu zitatolewa kwa wahusika kwa gharama.
Tutaitaja kesi hii Novemba 7, 2024 saa nane mchana katika mahakama ya wazi,” majaji walisema kwenye uamuzi huo uliosomwa na Jaji Ogola.
Chanzo: BBC
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Kanisa la AICT, Right to Play waadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike wakisisitiza haki ya elimu kwa wasichana
>>NECTA yatangaza matokeo ya darasa la saba 2024
>>Huyu ndiye Jenerali Musuguri kiboko wa dikteta Idi Amin wa Uganda, alipigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia 1939-1945 na Vita ya Kagera 1978-1979
>>Kura za maoni CCM: Mgombea alia kuhujumiwa kura Tarime Vijijini, akusudia kushitaki kwa Dkt Nchimbi
No comments:
Post a Comment