NEWS

Sunday, 17 November 2024

Majaliwa awatembelea majeruhi Muhimbili

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowatembelea majeruhi wa ajali ya ghorofa lililoporomoka Kariakoo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
                                                               ----------------------


NA MWANDISHI WETU, Dar
---------------------------------------

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana aliwatembelea majeruhi 40 waliolazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambao waliokolewa kwenye jengo lililoporomoka juzi katika eneo maarufu la biashara la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi alimwambia Waziri Mkuu kwamba majeruhi 35 waliruhusiwa kuondoka baada ya kufanyiwa uchunguzi wa afya zao na watano waliobaki wanaendelea na matibabu, wanne wakiwa chini ya uangalizi wa matibabu kwenye Taasisi ya Mifupa (MOI).

Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka ndugu wa watu walioumia kwenye ajali kuwa watulivu na kwamba serikali inashughulikia tiba ya majeuhi hao.

Eneo la Kariakoo, ambalo ni kitovu cha biashara kinachovutia maelfu ya watu mbalimbali kutoka nchi za jirani, katika miaka ya hivi karibuni limeshuhudia kuota kwa uyoga wa ujenzi wa maghorofa na kubadili mandhari ya jiji la Dar es Salaam.

Hata hivyo, wataalam wa ujenzi wanasema mrundikano wa maghorofa katika eneo moja ni hatari inapotokea ajali za moto na majanga mengine
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages