
Sehemu ya masalia ya mabati ya makazi ya familia ya Elias Ngare yaliyosombwa na mafuriko ya mto Mori mjini Tarime, Mara jana Novemba 24, 2024 usiku. (Picha na Joseph Maunya)
-------------------------------------
Watu tisa wa jinsia tofauti wa familia moja ya Elias Ngare, mkazi wa mjini Tarime, mkoani Mara wamefariki dunia baada ya makazi yao kuvamiwa na kusombwa na mafuriko ya mto Mori, unaotiririsha maji kwenda Ziwa Victoria nchini Tanzania.
Maafa hayo yalitokea jana Novemba 24, 2024 saa nne usiku katika mtaa wa Bugosi, katani Nyamisangura.

Sehemu ya mto Mori katika mtaa wa Bugosi.
Akizungumza na Mara Online News katika eneo la tukio hilo leo, Diwani wa Kata ya Nyamisangura, Thobias Elias Ghati amesema miili yote tisa imepatika na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Halmashauri ya mji wa Tarime, kilomita chache kutoka eneo la tukio.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Flowin Edward Gowele amethibitisha kutokea kwa maafa hayo ambayo pia yameacha watu kadhaa wa familia mbili bila makazi.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliyejitambusha kwa jina la Zacharia Ryoba Marwa ambaye pia ni jirani wa wahanga wa maafa hayo, amesema miji iliyosombwa na maji ni miwili na kwamba watu tisa wa familia Edward walinusurika licha ya kuachwa bila makazi.
Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara inatarajiwa kufika eneo la tukio wakati wowote leo kuanzia sasa, kwa mujibu wa vyanzo vyetu kutoka serikalini.
“Inasikitisha sana, polisi wamekuwa wakileta mili ya waliokufa katika hospitali ya Bomani tangu asubuhi,” amesema mmoja wa wakazi wa Tarime.
No comments:
Post a Comment