
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa (katikati waliokaa), viongozi wengine (waliokaa) na wadau wa uhifadhi na kilimo (waliosimama) wakati wa Mkutano Mkuu wa MRPC mjini Tarime jana Desemba 30, 2024.
-------------------------------------
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara umefanyika kwa mafanikio makubwa, huku viongozi na wadau mbalimbali wakikubaliana na waandishi hao kushirikiana katika kuchochea maendeleo ya mkoa huo.
Mbali na viongozi wa chama na serikali, wadau waliohudhuria mkutano huo ulioangazia uandishi bora kwa maendeleo ya jamii na uhifadhi endelevu, ni kutoka sekta za uhifadhi, madini na kilimo.
Wadau hao ni kutoka Hifadhi ya Taifa Serengeti (SENAPA), Grumeti Reserves, Grumeti Fund, Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara na Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa Mara (WAMACU Ltd).

Lengo kuu la mkutano huo uliofanyika mjini Tarime jana lilikuwa kuhamasisha uandishi wa habari za maendeleo ya kijamii na kiuchumi, yakiwemo yanayochagizwa na uhifadhi wa mazingira na wanyamapori, uchimbaji madini, kilimo, ufugaji na uvuvi katika mkoa wa Mara.

“Waandishi wa habari ni nguzo muhimu katika maendelei ya jamii na nchi yetu, tuna kila sababu ya kuendelea kuwatumia na kuwapa support (kuwawezesha),” alisema Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa aliyekuwa mgeni rasmi katika mkutano huo.

Mwenyekiti Chandi akizungumza
katika mkutano huo.
--------------------------------
Awali, Mwenyekiti wa MRPC, Jacob Mugini alihamasisha wanachama wa klabu hiyo kuongeza nguvu ya kuandika habari zinazotangaza fursa adimu na za kipekee zilizopo mkoani Mara.
Mugini akizungumza katika mkutano huo.
-----------------------------------
Mkutano huo ambao ulionesha mshikamano mkubwa kati ya wanahabari, serikali na wadau wa maendeleo, ulimalizika kwa azimio la kushirikiana kuandaa kongamano la kuutangaza zaidi mkoa wa Mara.
Picha zote na Mara Online News
Ni vizuri pia kusema eneo ambalo tukio limefanyika na mawasiliano ila wapata habari pia wajue Kwa manufaa mapana ya wapata habari . Mfano eneo au ukumbi ambalo MRPC wamefanya mkutano, au habari ya KSG Kurya social group in case mtu anataka kujiunga n.k hakuna mawasiliano
ReplyDelete