NEWS

Tuesday, 17 December 2024

Dkt Machage atembelea ofisi za Gazeti la Sauti ya Mara, alipongeza kwa kazi nzuri



Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Sauti ya Mara, Jacob Mugini (kushoto) akimkabidhi Dkt Edward Machage nakala ya gazeti hilo alipomtembelea ofisini kwake leo.
-----------------------------------

Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

Mdau wa maendeleo, Dkt Edward Machage, leo ametembelea ofisi za Gazeti la Sauti ya Mara na kupata fursa ya kuzungumza na wahariri wa gazeti hilo, Jacob Mugini na Christopher Gamaina.

Katika mazungumzo hayo, Dkt Machage amelipongeza gazeti hilo kwa kazi nzuri ya kuhabarisha jamii kuhusu miradi ya maendeleo ya kisekta inayotekelezwa na serikali katika mkoa wa Mara.

Pia, mdau huyo wa maendeleo ameahidi kuwa na ushirikiano wa karibu na chombo hicho cha habari kwa manufaa ya jamii nzima.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages