NEWS

Tuesday, 3 December 2024

Musoma Vijijini: Wanakijiji sasa waamua Nyasaungu Sekondari ifunguliwe Januari



Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo akizungumza na wananchi wakati wa maziko ya Steven Chacha Mwita Wambura kijijini Nyasaungu jana.
------------------------------


NA MWANDISHI WETU,Musoma
-------------------------------------------

WAKAZI wa kijiji cha Nyasaungu, jimbo la Musoma Vijijini wameamua kwa kauli moja kwamba shule ya sekondari mpya ya kijiji hicho ifunguliwe Januari 2025.

Walitoa azimio hilo kijijini hapo jana wakati wa maziko ya mmoja wa viongozi waanzilishi wa uchangiaji na ujenzi wa shule hiyo, Steven Chacha Mwita Wambura (1955-2024).

Chacha alikuwa maarufu kijijini Nyasaungu kwa kuwa mstari wa mbele katika kuchangia ujenzi wa shule ya msingi, shule ya sekondari Nyasaungu na zahanti ya kijiji hicho inayotarajiwa kufunguliwa wiki ijayo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini, mazishi ya mwanamaendeleo huyo yalihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Issa Chikoka, Mbunge wa jimbo hilo, Prof Sospeter Muhongo, Katibu Tawala wa Wilaya, Ally Seif Mwendo, wakazi wa Nyasaungu, vijiji vya jirani vya kata za Ifulifu, Nyakatende na Mugango, pamoja na marafiki, ndugu na jamaa kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Kufunguliwa mapema kwa Shule ya Sekondari Nyasaungu ni katika kumuenzi Chacha kwa msimamo wake wa kusaidia maendeleo ya kijiji hicho kwa hali na mali.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages