NEWS

Thursday, 16 January 2025

Dodoma: Makamu Mwenyekiti CCM Bara kujulikana mwishoni mwa wiki hii




Na Mwandishi Wetu

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) upande wa Tanzania Bara anatarajiwa kuchaguliwa katika Mkutano Mkuu wa chama hicho tawala utakaofanyika Januari 18 na 19, 2025 jijini Dodoma.

Nafasi hiyo ilikuwa wazi tangu Julai 2024 kutokana na kujiuzulu kwa aliyekuwa akiishikilia, Abdulrhaman Omar Kinana.

Kwa mujibu wa Katibu wa Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Amos Makalla, wajumbe wa mkutano huo watazungumzia ajenda tatu ambazo ni kumchagua Makamu Mwenyekiti CCM wa Tanzania Bara na kupokea taarifa za utkelekezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025.

Mada nyingine ni kupokea taarifa za utendaji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinmduzi ya Zanzibar.

Mkutano Mkuu wa CCM ndicho kikao cha juu zaidi cha chama hicho kikongwe barani Afrika, ambacho hutoa maamuzi ya uongozi wa nchi.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages