
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali, akiwemo Mhandisi Ramadhani Masoud Lwamo aliyemteua kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini nchini.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt Moses Kusiluka, Rais Samia pia amemteua Dkt Aggrey Kalimwage Mlimuka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ushindani (FCC) kwa kipindi cha pili.
Wengine ni Prof Othman Chande Othman aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kipindi cha pili na Dkt Florens Martin Turuka aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kwa kipindi cha pili.
Pia, Rais Samia amemteua Prof Valerian Cosmas Silayo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kwa kipindi cha pili, kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Sharifa Nyanga.
No comments:
Post a Comment