
Meneja Mkuu wa WAMACU Ltd, Samwel Gisiboye (aliyevaa suti ya kaki) akitoa maeleo ya kiwanda cha kuchataka kahawa kwa wakufunzi na wanafunzi kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi walipotembelea ushirika huo mjini Tarime leo Januari 14, 2025.
------------------------------------
Ujumbe wa wakufunzi na wanafunzi kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) umetembelea kiwanda cha kuchakata kahawa kinachomilikiwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa Mara (WAMACU Ltd), na kueleza kuridhishwa na kazi inayofanywa na ushirika huo katika kuhudumia wakulima wa kahawa na mazao mengine.
“WAMACU wameenda mbali zaidi kwa kufanya ushirika huu kuwa na kiwanda cha kuchakata kahawa, hivyo wakulima wanakuwa na uhakika wa soko la kuuza mazao yao, hasa kahawa,” kiongozi wa msafara wa ujumbe huo kutoka NDC, Brigedia Jenerali Baganchwera Rutambika amesema mara baada ya kutembelea kiwanda hicho mapema leo Januari 14, 2025.
Brigedia Jenerali Rutambika na ujumbe wake wamepata fursa ya kutembelea kiwanda hicho na kupata maelezo ya jinsi kinavyofanya kazi kutoka kwa Meneja Mkuu wa WAMACU Ltd, Samwel Gisiboye.
Aidha, aliupongeza ushirika huo kwa juhudi unazofanya katika kusambaza mbolea, mbegu na huduma za ugani kwa wakulima.

Ujumbe huo pia umeshuhudia makombe mbalimbali ambayo WAMACU Ltd imekuwa ikishinda kwa kuendelea kuzalisha kahawa bora aina ya Arabica ambayo inafanya vizuri katika soko la dunia.
Inaelezwa kuwa ushirika huo umepata mafaniko makubwa ya kuendelea kupanua wigo wa huduma zake kwa wakulima kutokana na uwezesho unaopata kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).
Meneja Mkuu wa WAMACU Ltd, Gisiboye, ameuomba ujumbe huo kutoka NDC kuwa mabalozi wazuri wa katika uwekezaji mkubwa katika kilimo nchini, ili kuinua uchumi wa wakulima wa chini.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya WAMACU Ltd, Momanyi Range amesema wamefarijika na ziara hiyo ya NDC katika ushirika huo.

Ujumbe wa wakufunzi na wanafunzi kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi wakiwa katika picha ya pmoja na viongozi wa WAMACU Ltd walipotembelea ushirika huo leo.
---------------------------------
Ujumbe huo wa NDC pia umetembelea Mgodi wa Dhahabu wa North Mara ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na mgodi huo ambao unaendeshwa na kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals.

Ujumbe wa wakufunzi na wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara leo.
----------------------------------
Mbali na Tanzania, wakufunzi na wanafunzi wa NDC wanatoka katika mataifa mbalimbali ya Africa kama vile Rwanda, Malawi, Zambia, Sierra Leone na Misri.
Taarifa zinasema ujumbe huo wa NDC upo katika ziara ya siku tano mkoani Mara, ambapo jana ulikutana na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi ofisini kwake mjini Musoma.
No comments:
Post a Comment