
Mbunge wa Jimbo la Serengeti, Jeremiah Mrimi Amsabi (katikati) na wananchi wa kata ya Kenyamonta wakifurahi wakati wa makabidhiano ya gari la wagonjwa juzi.
--------------------------------------
Hatimaye tatizo lililokuwa likiwakabili wananchi wa kata ya Kenyamonta wilayani Serengeti, Mara, la ukosefu wa gari la kusafirisha wagonjwa kwenda Kituo cha Afya Iramba, limepatiwa ufumbuzi.
Ufumbuzi wa tatizo umetokana na juhudi za Mbunge wa Jimbo la Serengeti, Jeremiah Mrimi Amsabi, ambapo juzi alikabidhi gari hilo katika hafla iliyofanyika kwenye Kituo cha Iramba, ili liwahudumie wakazi wa kata hiyo na vijiji jirani.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Dkt Lusubilo Adam, viongozi wa serikali na chama tawala - CCM, na wananchi wanaohudumiwa na kituo hicho.
Mbunge Amsabi alitilia mkazo matumizi bora na utunzaji wa gari hilo ili liendelee kuwahudumia wananchi wengi zaidi.
Naye Mganga Mkuu akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Dkt Lusubilo aliahidi kusimamia uongozi wa Kituo cha Iramba ili kuhakikisha gari hilo linatumika kwa shughuli zilizokusidiwa.
Aliishukuru serikali kwa jitihada zake za kuboresha sekta ya afya wilayani Serengeti ili kuwezesha wananchi kupata huduma bora.
Wananchi wa kata ya Kenyamonta nao waliipongeza serikali kwa kuboresha huduma za afya na kuondoa changamoto ya ukosefu wa gari la wagonjwa iliyokuwa ikiwakabili, hasa wajawazito waaliohitaji kuwahishwa hospitalini.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Tanzania, Uingereza kushirikiana kuwajengea wananchi uwezo sekta ya madini
>>Mara: Maelfu ya wanafunzi wapata 0 za kutisha Mtihani wa Taifa Kidato cha Pili 2024
>>MAKALA MAALUMU:Bunda: Wananchi wajenga barabara ya kwanza kisiwani Nafuba, Dkt Mukama na wadau wengine wawapiga jeki
>>MAKALA YA UCHAMBUZI:Dkt Machage apewe maua yake kwa moyo wa kujali afya za wananchi Tarime Vijijini
No comments:
Post a Comment