![]() |
Leonard Mambo Mbotela enzi za uhai ------------------------------------- |
Tasnia ya habari nchini Kenya inaomboleza kifo cha mwanahabari nguli Leonard Mambo Mbotela aliyefariki akiwa na umri wa miaka 88.
Mbotela amefanya kazi ya uandishi wa habari kwa zaidi ya miongo mitano, lakini tukio lililoandikisha historia katika maisha yake ni jaribio la mapinduzi ya mwaka 1982 ambapo baadhi ya wanajeshi wakati huo walitaka kumuondoa madarakani aliyekuwa Rais wa wakati huo Daniel Arap Moi.
Wanajeshi hao waasi walimchukua nyumbani kwake na kumpeleka katika kituo cha redio cha Sauti ya Kenya (VOK) na kumlazimisha atangaze kuwa serikali ya Rais Moi imepinduliwa.
Pia, atakumbukwa kwa kipindi chake cha 'Jee Huu ni Ungwana' alichokifanya kwa ucheshi uliowakonga mioyo wasikilizaji wake na ambacho kilipeperushwa hewani kwenye Redio na ma baadaye kwenye Televisheni ya Shirika la Utangazaji la Kenya KBC.
Kipindi hicho kilianzishwa mwaka 1966 na kilipeperushwa hewani kwa takriban miaka 55.
Chanzo: BBC
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Nyambari Nyangwine Foundation yaendelea kusambaza msaada wa vitabu sekondari za Tarime Vijijini
>>Aga Khan IV afariki dunia nchini Ureno
>>HABARI PICHA:Wasira kuzuru wilaya za Rorya, Tarime na Serengeti
>>Mkutano Mkuu WAMACU wapitisha ununuzi kiwanda cha chai, RC awapongeza kwa kuitangaza kahawa ya Tarime
No comments:
Post a Comment