
Shule ya Sekondari Magoto iliyopo kata ya Nyakonga wakipokea msaada wa vitabu uliotolewa na Nyambari Nyangwine Foundation jana Februari 20,2025.
----------------------------------
Taasisi ya Nyambari Nyangwine Foundation (NNF) imehitimisha awamu nyingine ya usambazaji wa msaada wa vitabu vya kiada na ziada kwenye shule nne za sekondari zilizopo kata za Nyakonga, Nyansincha na Ganyange katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini).
Shule hizo ni Nyantira (Nyansincha), Magoto (Nyakonga), Ganyange na Borega ya Wasichana yenye kidato cha kwanza hadi cha sita (Ganyange) zilikabidhiwa msaada wa vitabu hivyo jana Februari 20, 2025 na wawakilishi wa NNF, Sospeter Migera Paul na Chacha Ambrose Nyangoko.

Makabidhiano ya vitabu katika
Shule ya Sekondari Borega.
---------------------------------

Makabidhiano ya vitabu katika
Shule ya Sekondari Ganyange.
---------------------------------

Makabidhiano ya vitabu katika
Shule ya Sekondari Nyantira.
-------------------------------
Nyambari Nyangwine Foundation imeweza kusambaza msaada wa vitabu kwenye shule za sekondari zilizopo katika halmashauri za Wilaya ya Tarime (Vijijini) na Tarime Mjini, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali za uboreshaji wa taaluma kwa wanafunzi.
No comments:
Post a Comment