NEWS

Friday, 21 February 2025

Nairobi: Aliyekuwa Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati afariki dunia



Wafula Chebukati enzi za uhai

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) nchini Kenya, Wafula Chebukati, amefariki dunia.

Chebukati alikuwa amelazwa katika hospitali moja jijini Nairobi katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Kulingana na familia, Chebukati aliaga dunia Alhamisi, Februari 20, 2025 saa 11 jioni alipokuwa akipata matibabu.

Bosi huyo wa zamani wa IEBC alikuwa amelazwa katika hospitali moja jijini Nairobi ambapo amekuwa akitibiwa kwa takriban wiki moja katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Chebukati alihudumu kama Mwenyekiti wa IEBC kwa muhula mzima wa miaka sita, ambapo alisimamia Uchaguzi Mkuu Kenya mara mbili kabla ya kustaafu Januari 2023.

Aliongoza Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2017 ambapo Rais wa zamani, Uhuru Kenyatta alimshinda mgombea urais wa CORD, Raila Odinga.

Chebukati pia aliongoza Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2022 uliokuwa na ushindani mkubwa, ambapo Rais William Ruto alitangazwa mshindi.
Chanzo: TUKO Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages