
Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyamwaga, Emmanuel Gabriel Wankaba na wanafunzi wa Shule ya Sekondari JK Nyerere wakionesha msaada wa vitabu waliopokea kutoka Taasisi ya Nyambari Nyangwine jana Februari 17, 2025.
-------------------------------------
Taasisi ya Nyambari Nyangwine (NNF) imeendelea kusambaza msaada wa vitabu vya kiada na ziada kwenye shule za sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini), ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali za uboreshaji wa taaluma kwa wanafunzi.
Ambapo jana Februari 17, 2025 Mwakilishi wa NNF, Sospeter Migera Paul alikabidhi msaada huo katika sekondari za Nyamwaga, Genge, Bwirege, Nyarero na JK Nyerere yenye kidato cha kwanza hadi cha sita.

Makabidhiano ya msaada wa vitabu
katika Shule ya Sekondari Nyarero.
---------------------------------------

Makabidhiano ya msaada wa vitabu
katika Shule ya Sekondari Bwirege.
----------------------------------------
Wakizungumza katika hafla za kukabidhi vitabu hivyo, walimu, wanafunzi na viongozi wa vijiji na kata zilipo shule hizo walishukuru na kumtaja Nyambari Nyangwine kama mwanamaendeleo wa kweli.
“Huyu Nyambari Nyangwine huwa anajitolea sana, hii ni mara ya pili kutusaidia vitabu, watoto mjitahidi kusoma Kwa bidii,” alisema Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nyarero, Makoba Mohabe Mohere.

Makabidhiano ya msaada wa vitabu
katika Shule ya Sekondari Genge.
---------------------------------------
Naye Diwani wa Kata ya Nyamwaga, Mwita Magige alisema: “Ninawapenda watu wa aina hii [Nyambari Nyangwine] wanaosaidia jamii.”
Awamu hii ya usambazaji wa msaada huo wa vitabu ilianza mwaka jana katika Halmashauri ya Mji wa Tarime kisha kuendelea Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini).

Makabidhiano ya msaada wa vitabu katika Shule ya Sekondari Nyamwaga. (Picha zote na Mara Online News)
----------------------------------------
No comments:
Post a Comment