NEWS

Wednesday, 19 February 2025

Ujumbe wa JWTZ wafanya ziara Mara



Mkuu wa wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi (katikati waliokaa) akiwa na ujumbe wa JWTZ uliotembelea mjini Musoma jana.
-----------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Musoma

Ujumbe wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ukiongozwa na Mkuu wa Utumishi wa jeshi hilo, Meja Jenerali Marco Gaguti, juzi ulianza ziara ya siku mbili ya kikazi mkoani Mara.

Jana, ujumbe huo ulifanya mazungumzo na Mkuu wa wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, kuhusu masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama.

Kanali Mtambi aliuhakikishia ujumbe huo kuwa mkoa wa Mara ni shwari na shughuli zote za maendeleo zinafanyika kawaida huku wananchi wakifurahia maisha.

Alilipongeza JWTZ kwa kazi kubwa ya ulinzi wa taifa na kutoa ushirikiano kwa mkoa wa Mara katika kuhakikisha kunakuwepo amani na usalama.

Naye Meja Jenerali Gaguti alimshukuru Kanali Mtambi kwa ushirikiano unaotolewa na mkoa wa Mara kwa shughuli za JWTZ.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages