NEWS

Friday, 14 February 2025

Kata za Mwema, Susuni, Bumera zafikiwa na msaada wa vitabu vya sekondari kutoka Nyambari Nyangwine Foundation



Walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwema wakipokea msaada wa vitabu kutoka kwa mwakilishi wa Nyambari Nyangwine Foundation, Sospeter Migera Paul (kushoto) jana Februari 13, 2025.
------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Tarime

Shule za sekondari Kurumwa, Bumera, Mwema, Korotambe na Nyabirongo zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) zimepokea msaada wa vitabu vya kiada na ziada kutoka Nyambari Nyangwine Foundation (NNF).

Huo ni mwendelezo wa taasisi hiyo wa kusambaza msaada wa vitabu kwenye sekondari tano kila siku.

Makabidhiano ya vitabu katika 
Shule ya Sekondari Korotambe.
-------------------------------------

Mwakilishi wa taasisi hiyo, Sospeter Migera Paul alikabidhi msaada huo wa vitabu kwa kwa walimu na wanafunzi wa shule hizo kwa nyakati tofauti jana Februari 13, 2025.

Walimu na wanafunzi waliishukuru Taasisi ya Nyambari Nyangwine wakisema vitabu hivyo vitakuwa chachu ya maendeleo ya kitaaluma katika shule hizo.


Makabidhiano ya vitabu katika 
Shule ya Sekondari Nyabirongo.
-------------------------------------


Makabidhiano ya vitabu katika 
Shule ya Sekondari Kurumwa.
------------------------------------

Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kurumwa iliyopo kata ya Bumera, Joseph Marwa Kisiri,akitoa neno la shkrani ameutaja msaada huo kama bahati kwao na kuahidi kusoma kwa bidii

"Hii ni bahati kwetu, tunaahidi matokeo mazuri katika mitihani yetu," mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kurumwa, Joseph Marwa Kisiri alisema.

Mwanafunzi Joseph Marwa Kisiri (katikati)
---------------------------------

Msaada wa vitabu kwa shule za sekondari unaotolewa na Taasisi ya Nyambari Nyangwine ni sehemu ya kuunga juhudi za serikali za uwekezaji na uboreshaji wa elimu nchini kwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata vifaa muhimu vya kujifunzia ili waweze kufikia ndoto zao za elimu.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages