NEWS

Thursday, 27 March 2025

Afisa Tarafa (Mstaafu) Machango aliyehudumu wilayani Tarime kwa miaka mingi afariki dunia



Jonathan Machango enzi za uhai

Na Mwandishi Wetu, Tarime

Aliyewahi kuwa Afisa Tarafa katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Tarime, ikiwemo tarafa ya Inchage, Jonathan Machango, amefariki Dunia.

Machango ameaga dunia leo Machi 27, 2025 katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza alipokuwa akipata matibabu, kwa mujibu vyanzo vyetu vya uhakika kutoka kwa wanafamilia.

Watu wa kada mbalimbali wanamuelezea Machango - maarufu kwa jina la Aiko, kama mtu aliyekuwa kiongozi mchapa kazi na mwadilifu.

Alihudumu kwa muda mrefu kama Katibu/ Afisa Tarafa wa Inchage na alionekana kuwa kiongozi aliyeaminiwa na mabosi wake, yaani wakuu wa wilaya wote aliowahi kufanya nao kazi.

“Alikuwa kiongozi mcheshi, hakuwa na majivuno,” amesema Mkurugenzi na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Mara Online, Jacob Mugini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klub ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara Jacob.

Watu mbalimbali wameendelea kutuma salamu za rambirambi kwa familia, wakieleza kushitushwa na kifo cha mzee Machango.

“Poleni sana familia ya mzee wetu Jonahan Machango kwa kuondokewa na mzee huyu, nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi makubwa, sisi umoja wa wafanyabiashara wa Tarime tumeondokewa na mwenyekiti wetu,” ameandika Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Lucas Ngoto, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook.

Taratibu za mazishi zitatolewa na familia.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages