
Daniel Chonchorio Nyamhanga
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Mfanyabiashara wa jijini Mwanza, Daniel Chonchorio Nyamhanga, 46, ameripotiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha baada ya kuaga familia yake asubuhi ya Jumapili Machi 23, 2025, kwamba anakwenda kufanya mazoezi ya viungo.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza jana Jumatatu inaeleza kuwa mfanyabiashara huyo, ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Temeke katika kata ya Nyakato, wilayani Nyamagana aliondoka nyumbani kwake saa mbili asubuhi akiwa amevaa nguo za mazoezi na simu ya mkononi.
Wanafamilia wa Chonchorio walioripoti polisi tukio la kutowekwa kwake walisema hadi kufikia muda wa saa tano asubuhi siku hiyo, ndugu yao hakurudi nyumbani hali iliyowafanya kuiingiwa wasiwasi na kulazimika kutoa taarifa kwa chombo hicho cha usalama wa raia na mali zao.
Taarifa inaeleza kuwa Jeshi la Polisi mara moja lilianza uchunguzi wa tukio hilo kwa kuwahusisha wanafamilia, ndugu, marafiki na majirani wa Chonchorio.
Hata hivyo, taarifa hiyo inaeleza kuwa hadi jana mfanyabiashara huyo alikuwa hajapatikana.
Chonchorio pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa mwenye makazi mengine katika mji wa Tarime mkoani Mara na jijini Dar es Salaam.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
»Mwenyekiti UVCCM Mara awataka vijana wa umoja huo kuepuka vitendo vinavyochafua chama
»Tarime Vijijini: Wananchi Nyanungu walia ubovu wa barabara ya kwenda zahanati ya Nyandage
»Nyambari Nyangwine kufadhili semina ya washairi wa Tanzania ili kuboresha ufanisi wao
»Serengeti: Mwenyekiti UVCCM Mara aunga mkono Serikali kufanikisha upatikanaji wa lishe mashuleni
No comments:
Post a Comment