NEWS

Thursday, 27 March 2025

Mwenyekiti UVCCM Mara awasilisha changamoto za vijana ofisi za UNFPA jijini Dar es Salaam



Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mara, Mary Daniel Joseph (kushoto) na Tausi Hassan wa Idara ya Vijana ya Shirika la UNFPA jijini Dar es Salaam wakifurahia picha ya pamoja baada ya kufanya mazungumzo maalum leo Machi 27, 2025.
----------------------------------------

Na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mara, Mary Daniel Joseph, leo Machi 27, 2025, ametembelea ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA) zilizopo jijini Dar es Salaam, ambapo amekutana na kufanya mazungumzo maalum na Tausi Hassan wa Idara ya Vijana ya shirika hilo.

Katika mazungumzo hayo, Mary ameeleza changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana wa Mkoa wa Mara, sambamba na kuomba ushirikiano na Idara ya Vijana ya UNFPA ili kuwainua vijana wa mkoa huo na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages