NEWS

Sunday, 9 March 2025

IDS waadhimisha Siku ya Wanawake kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia Tarime Vijijini




Na Godfrey Marwa, Tarime

Shirika la Inland Development Services (IDS) limeadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, miongoni mwa shughuli nyingine katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, mkoani Mara.

Katika uhamasishaji huo, wameonesha faida za majiko banifu yanayotumia kuni chache, hatua inayosaidia kupunguza athari za kiafya na kulinda mazingira.

Maadhimisho hayo yalifanyika jana Machi 8, 2025 katika kata ya Nyakonga, wakiwaleta pamoja wanawake walio kwenye vikundi, na wanafunzi wa kike kutoka Shule ya Msingi Magoto.

Awali, walipanda miti ya matunda shuleni hapo ili kukuza uhifadhi wa mazingira na kuwezesha upatikanaji wa lishe bora kwa jamii.

Pamoja na mambo mengine, maadhimisho hayo yalihusisha majadiliano juu ya umhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kupitia mradi wa Asili B unaofadhiliwa na Shirika la Vi-Agroforestry.

Lengo ni kuunga mkono jutihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan katika kumkomboa mwanamke dhidi ya matumizi ya nishati ya isiyo rafiki kiafya na mazingira.

"IDS tumeona ni vizuri kwenye hii Siku ya Wanawake Duniani kushiriki katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kuwafundisha kutengeneza wa majiko banifu ambayo ni rafiki kiafya na mazingira,"

Aliongeza: "Pia, tunahamasisha upandaji miti ambayo ni rafiki kwa mazingira, ikiwemo ya matunda Pamoja na bustani ya mboga mboga, na hatimaye kuboresha maisha ya mkulima mdogo kiuchumi kwa kuzingatia mbinu bora za kilimo, ikiwa ni pamoja na kuzingatia kilimo mseto."



IDS ilitumia fursa hiyo pia kutoa elimu muhimu kwa vikundi vya wanawake na wanafunzi kuhusu haki za wanawake.

Mwanachama wa kikundi cha juhudi na maarifa, Scolastica Samson Nyansiri alisema: "Kupitia majadiliano haya nimejitambua kuwa mimi ni mwanamke mwenye thamani sana, serikali na mashirika yathamini mchango wa mwanamke, wanawake ndio walezi - wakiwezeshwa utakuwa umeimarisha familia na taifa."

Kwa upande mwingine, wanafunzi wa kike kutoka Shule ya Msingi Magoto walipongeza shirika la IDS kwa kuwajumuisha katika maadhimisho hayo, kwani wamepata elimu ya umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia na wameahidi kuwa mabalozi wema katika jamii.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages