NEWS

Sunday, 9 March 2025

Tarime: Nyambari achangisha shilingi milioni 45.6 KMT Mangucha, SDA Nyabitocho



Askofu Amos Mohagaji wa Kanisa la Mennonite Dayosisi ya Shirati akimshukuru Nyambari Nyangwine (aliyevaa kofia) kwa kufanikisha harambee ya kuchangia katika Kanisa la Mennonite Mangucha katani Nyanungu.
---------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Tarime

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime, Nyambari Nyangwine ameendesha harambee katika Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT) lililopo kijiji cha Mangucha katika kata ya Nyanungu wilayani Tarime na kufanikisha kupatikana kwa shilingi zaidi ya milioni 27.

Katika harambee hiyo iliyofanyika kanisani hapo jana, Nyambari mwenyewe alichangia shilingi milioni 10, ambapo pia alisindikizwa na rafiki zake, wakiwemo madiwani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini).

Diwani wa Kata ya Nyanungu, Tiboche Richard alishiriki katika harambee hiyo ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo.

Pia, Nyambari aliahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 12 kuchangia makanisa mbalimbali yaliyopo katani hapo.

“Mimi ni mzaliwa wa kata hii, nitachangia maendeleo ya makanisa mengine manne, kila kanisa nitalichangia shilingi milioni tatu,” Nyambari ambaye pia ni mfanyabiasha, mwandishi na mchapishaji wa vitabu maarufu nchini Tanzania, aliwambia waumuni wa kanisa hilo na kuibua shangwe na vigelegele.

Makanisa yatakayonufaika na mchango huo ni Romani Katoliki, Anglikana, KKKT na SDA.


Katika hotuba yake kwenye harambee hiyo, Nyambari aliwahimiza wananchi wa wilaya ya Tarime kuwa na upendo na kuendelea kudumisha amani.

Aidha, Nyambari aliwataka wananchi wa kata hiyo na wilaya kwa ujumla kuwekeza katika elimu na kulipa kipaumbele suala la elimu ya ujasiriamali.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Askofu wa KMT Dayosisi ya Tarime, Albert Jera Randa na Askofu Amos Joseph Muhagachi wa KMT Dayosisi ya Shirati.


Viongozi wa dini wakimkabidhi Nyambari Nyangwine cheti cha pongezi,
------------------------------------

Harambee hiyo ilifanyika siku moja baada ya Nyambari kuendesha harambee nyingine katika Kanisa la SDA Nyabitocho na kufanikisha kupatikana kwa shilingi milioni 18.6, ambapo yeye mwenyewe alichangia shilingi zaidi ya milioni 10.

Akiwa katika changisho la Nyabitocho SDA, Nyambari pia alitangaza kuchangia shilingi milioni mbili katika kanisa jirani la SDA Kyoruba Mlimani.

Siku hiyo hiyo, Nyambari alifika katika Kanisa la EAGT Sirari na kuichangia kwaya ya kanisa hilo shilingi milioni mbili.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages