NEWS

Sunday, 9 March 2025

Nyambari ahimiza upendo Tarime, achangisha milioni 18.6/- Kanisa la SDA Nyabitocho



Mchungaji wa Kanaisa la SDA Mtaa wa Nyabitocho, Kumba Kihiri (kulia) akipokea kutoka kwa Nyambari Nyangwine mchango wa shilingi milioni tano taslimu kwa ajili ya ujenzi wa kibweta cha makambi cha kanisa hilo jana.
---------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Tarime

Mfanyabiashara, mwandishi na mchapishaji wa vitabu maarufu nchini, Nyambari Nyangwine amewahimiza wananchi wa wilaya ya Tarime, mkoani Mara kudumisha upendo, umoja na mshikamano kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Nyambari aliyasema hayo jana Jumamosi wakati wa harambee ya ujenzi wa kibweta cha makambi cha Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) Nyabitocho katani Mbogi, ambapo alikuwa mgeni rasmi.

"Tushikamane tuwe kitu kimoja sisi kama wana-Tarime, ndiyo maana nasisitiza upendo kwa maana hayo mengine yote yanapita," alisema Nyambari ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime Kwa chama tawala - CCM.

Katika harembee hiyo, Nyambari alichangisha shilingi milioni 18.6, ambapo mwenyewe alichangia fedha taslimu shilingi milioni tano na kuahidi kutoa shilingi milioni tano nyingine.

"Leo naanza kuwachangia milioni tano cash (taslimu), lakini pia mtanipa akaunti yenu niweke milioni tano nyingine… tushikamane tuifanye Tarime kuwa mahali salama," alisema Nyambari.


Madiwani wakimsindikiza Nyambari Nyangwine kwa uchangiaji katika harambee hiyo.
------------------------------------

Aidha, Nyambari alisindikizwa na rafiki zake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini), Simion Kiles ambaye alitoa shilingi milioni moja, Mkurugenzi wa Mara Online, Mugini Jacob (shilingi 200,000) na baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo (shilingi 900,000).

Kwa upande mwingine, Nyambari alitoa shilingi milioni moja kwa kikundi cha sanaa kiitwacho Nyakonga Film Group na kukiahidi mwaliko wa kukutana nacho jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuongeza ujuzi zaidi.

Awali, Nyambari alililipatia Kanisa la EAGT Sirari Bondeni mchango wa shilingi milioni mbili kwa ajili ya ununuzi wa vyombo vya muziki vya kwaya ya kanisa hilo.


Nyambari Nyangwine akipokewa na kuvishwa skafu katika Kanisa la SDA Nyabitocho
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages