
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto) akifurahia baadaya kumtwisha mama ndoo ya maji wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wilayani Igunga, Tabora jana. Katikati ni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.
-------------------------------
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, jana Machi 12, 2025, aliweka jiwe la msingi la mradi wa mtandao wa majisafi ya Ziwa Victoria kutoka eneo la Makomero-Mgongoro, wilayani Igunga, Tabora.
Mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 840.8 unalenga kuwanufaisha wananchi 5,000 kwa huduma ya majisafi na salama.
Baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo, Waziri Mkuu Majaliwa alisema serikali itaendelea kusimamia utoaji wa huduma ya maji na kuhakikisha kuwa upatikanaji wake unafikia asilimia 100.
Aliiagiza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kusogeza vituo vya umma vya kuchota maji karibu na wananchi.
Ujenzi wa mradi huo kwa sasa umefikia asilimia 80 na unahusisha vituo sita vya umma vya kuchota maji, ukarabati wa mabirika mawili ya maji ya mifugo, kuchimba mitaro ya kulaza bomba na mitaro mita 25,000.
Naye Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, akizungumza kwenye hafla hiyo, aliwataka wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha wanatenda haki na kuaepuka kuwabambikizia wananchi ankara za maji.
Aweso alisema dhamira ya serikali ni kuhakikisha huduma ya upatikanaji wa maji inawafikia wananchi wengi zaidi nchini.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
»Wasira aanza ziara ya kukagua shughuli za CCM SongweMPYA
»Manga Sekondari yapokea msaada wa photocopy machine, kompyuta 3 ikisherehekea Mahafali ya Kidato cha Sita 2025
»Tarime: Sinda amuunga mkono Nyambari uchangiaji fedha za ununuzi vifaa vya kwaya ya EAGT Sirari Bondeni
»MAKALA YA UCHAMBUZI:Nyambari Nyangwine ameonesha moyo wa kujitolea na upendo mkubwa katika ujenzi wa makanisa Tarime
No comments:
Post a Comment