
Mwenyekiti wa UVCCM) Mkoa wa Mara, Mary Daniel, akizungumza na vijana wa umoja huo wilayani Tarime wiki iliyopita.
---------------------------------
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mara, Mary Daniel, amewataka vijana wake kuepuka vitendo vinavyoweza kuchafua picha ya umoja huo, badala yake wawe tayari kutetea na kusaidia wanapohitajika ili kujijengea heshima wakati wote.
Mary alitoa kauli hiyo alipozungumza na vijana wilayani Tarime wiki iliyopita wakati wa kuhitimisha ziara yake ya kusikiliza za na kutatua kero mbalimbali za vijana na makundi mengine katika mkoa wa Mara.

Sehemu ya vijana wa UVCCM wakifuatilia hotuba ya mwenyekiti wao katika mkutano huo.
----------------------------------------
“Hatuna sababu ya kuwa tunadanganyana ama tunatiana moyo - tunakichafua chama kwa sababu tu sisi ni moja kati ya jumuiya zake imara. Sisi kuwa vijana wa Chama Cha Mapinduzi haitupi upendeleo wowote wa sisi kuvunja sheria na kwenda kinyume na utaratibu,” alisema Mary.
Aliwaomba vijana hao kujenga utamaduni wa kutii sheria bila shuruti, na pale itakapooneka yeyote ameonewa wasimame pamoja na kutumia utaratibu unaokubalika kutafufuta ufumbuzi.
“Tukiendelea kudanganyana kwamba kwa vile wewe ni kijana wa Chama Cha Mapinduzi fanya hiki hautakutwa na chochote, huo ni uongo, kwa sababu wakati wewe unafanya hivyo na mtu mwingine atatumia mgongo huo huo atafanya baya kubwa atasingizia na yeye ni kijana wa Umoja wa Vijana, mwisho wa siku wote tunakuwa tunaonekana hatuna maana,” Mary alisisitiza.
Huku akihamasisha kaulimbiu ya sasa inayosema “Kazi na Utu, Tunasonga Mbele”, Mary aliwahimiza vijana wa UVCCM kuhakikisha wanafuata utaratibu na kuwa mfano bora ili kulinda heshima ya umoja huo na CCM kwa ujumla.

Mwenyekiti huyo wa UVCCM Mkoa wa Mara alihitimisha kwa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa maendeleo makubwa aliyofanya ndani na nje ya chama hicho, kwa manufaa ya Watanzania kwa ujumla.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
»Mfanyabiashara na Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM aripotiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha
»Tarime Vijijini: Wananchi Nyanungu walia ubovu wa barabara ya kwenda zahanati ya Nyandage
»Nyambari Nyangwine kufadhili semina ya washairi wa Tanzania ili kuboresha ufanisi wao
»Namibia yamuapisha Rais wake wa kwanza mwanamke, Rais Samia ampongeza
No comments:
Post a Comment