NEWS

Monday, 3 March 2025

Tarime Mjini: Washindi Matiko Cup wajazwa mamilioni ya fedha



Kepteni wa Nyamisangura FC akionesha shilingi milioni 15 ambazo timu hiyo imezawadiwa baadaya kuibuka mshindi wa Matiko Cup 2024/2025.
----------------------------------


Kepteni wa Nyamisangura FC iliyoibuka mshindi wa Matiko Cup, akikabidhiwa kombe katika uwanja wa Serengeti mjini Tarime jana Machi 2, 2025.
----------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Tarime

Washindi wa Matiko Cup 2024/2025 katika Halmashauri ya Mji wa Tarime, mkoani Mara wamekabidhiwa zawadi zao, zikiwemo fedha taslimu kutoka kwa mdhamini mkuu wa mashindano hayo, Matiko Foundation.

Mashindano hayo yalihusisha mpira wa miguu, pool, drafti, detis, bao na kuchoma nyama.

Kwa upande wa mpira wa miguu, timu ya Nyamisangura FC imezawadiwa kombe na shilingi milioni 15 na mshindi wa pili, Giants FC amepewa shilingi milioni 10.

Mshindi wa tatu, HAMTA FC alikabidhiwa shilingi milioni tano, mshindi wa nne, Tarime United FC shilingi milioni mbili, huku timu nyingine zote zilizoshiriki zikiambulia kila moja shilingi laki tano.


Wachezaji wa timu ya Nyamisangura FC katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali baada ya kukabidhiwa zawadi kwa kuibuka mshindi wa Matiko Cup 2024/2025.
------------------------------------

Makabidhiadho ya zawadi hizo yalifanyika jana Machi 2, 2025 katika uwanja wa Serengeti “Shamba la Bibi” mjini Tarime, ambapo mgeni rasmi alikuwa, Samwel Kiboye “Namba Tatu” ambaye aliwapongeza washindi na washiriki wote wa mashindano hayo.

Mwenyekiti wa Matiko Foundation, Esther Matiko ambaye pia Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, aliwashukuru wadau waliomuunga mkono katika kufanikisha mashindano hayo.

"Nishukuru wadau mbalimbali walioshirikiana na Matiko Foundation, tulianzisha taasisi hii kwa ajili ya kurudisha fadhila kwa wananchi wa Tarime, mliamua kuondoa mfumo dume nikawa mbunge mwanamke wa kwanza kuchaaguliwa,” alisema Mbunge Matiko.

Aliongeza: “Matiko Foundation itaendelea kuwalipa fadhila, kwenye michezo ni lazima tuunge juhudi za Mama Dkt Samia Suluhu Hassan [Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages