NEWS

Saturday, 1 March 2025

Mwandishi Azam Tv ashinda Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kutoka Mara










Augustine Mgendi

Na Mwandishi Wetu, Musoma
Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Azam Media Ltd Mkoa wa Mara, Augustine Mgendi amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutoka Mkoa wa Mara.

Katika uchaguzli huo uliofanyika leo March 1, 2025 mjini Musoma, Mgendi ameibuka mshindi baada ya kupata kura tano dhidi ya mshindani wake wa karibu, Revocatus Kuboja aliyepata kura nne.

Kwa upande wake Mussa Nyamandege aliyekuwa mgombea pekee, amethibitishwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM).

Baada ya uchaguzi huo, mwenyekiti mteule huyo wa FAM amemteua Haroub Salum kuwa makamu wake.
Read Also Section Example

UNAWEZA PIA KUSOMA:

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages