
Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi (aliyevaa shati la kijani), akikagua maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege Musoma, mkoani Mara leo Aprili 23, 2025. Wengine ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa (aliyevaa shati la njano), Mkuu wa Mkoa huo, Kanali Evans Alfred Mtambi (aliyevaa suti nyeusi) na Meneja wa TANROADS Mkoa, Mhandisi Vedastus Maribe (aliyenyoosha mkono akitoa maelezo ya mradi huo), miongoni mwa viongozi wengine wa chama na serikali.
---------------------------------------
Kwa mujibu wa Mhandisi Maribe, mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya shilingi zaidi ya bilioni 35 kutoka Serikali ya Tanzania.
Uwanja huo ukikamilika utakuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa mkoa wa Mara, ambapo utawezesha watalii kutoka maeneo mbalimbali kutua kabla ya kwenda kutembelea Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mara, Mhandisi Vedastus Maribe, akimuonesha Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi (kulia), ramani na maelezo ya mradi wa ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege Musoma. Wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa.

Balozi Dkt Nchimbi anaendelea na ziara yake ya siku tano ya ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025 katika mkoa wa Mara iliyoanza jana Aprili 22, 2025.
Mara Online News itaendelea kukufahamisha habari zaidi kuhusu ziara ya kiongozi huyo wa chama tawala - CCM inayoendelea mkoani Mara.
No comments:
Post a Comment