
Papa Francis enzi za uhai
Na Mwandishi Wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, ameeleza kusikitishwa na taarifa ya kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francisko, kilichotokea leo Jumatatu ya Pasaka Aprili 21, 2025.
“Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatuma salamu za pole kwa waumini wote wa Kanisa Katoliki hapa nchini na duniani kote.
“Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina,” Rais Samia ameandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii leo.

Rais Samia akizungumza na Papa Francis alipofanya ziara Vatican, Februari 2024,
Mapema leo Jumatatu ya Pasaka, Mwadhama, Kardinali Farrell, ametangaza kwa masikitiko kifo cha Baba Mtakatifu Francis, akisema amefariki dunia leo saa 7:35 asubuhi (kwa saa za huko) katika makazi yake yaliyopo Casa Santa Marta, Vatican akiwa na umri wa miaka 88.
Kifo cha Papa kimekuja chini ya saa 24 baada ya kujitokeza kwenye Uwanja wa St Peter's Square mjini Vatican kwa ajili ya Jumapili ya Pasaka jana.
Papa Francis alitoka akiwa kwenye kiti cha magurudumu na kupunga mkono kutoka kwenye baraza ya Basilica ya St Peter's kwa umati wa watu waliokuwa wakishangilia na kusema: "Ndugu wapendwa, Pasaka njema."
No comments:
Post a Comment